Breaking News

ASANTE KWASI ANAPOWAPA SOMA WASHAMBULIAJI


Na *Saidi Mwalimu Jr*

Wakati mwingine mchezo wa soka unaweza kusema ni wa maajabu au unaweza kusema kama mtu anajua amejua.Naam hayo hayapingiki licha ya hayo siri ya mafanikio ya soka ni Nidhaku,Kujituma ( chachu ya mafanikio) na kuwa na subira.
Katika kitu ambacho kwa sasa nikionacho katika timu ya simba ni uwezo wa mtu kama Asante Kwasi,Kwasi nilishawahi kumzungumzia hapo nyuma ( nagusia kidogo).Simba imeweza kunufaika na asante kwasi katika upande wa kushambulia zaidi kuliko kujilinda,asante kwasi asili yake ni beki wa kati na simba wakati wanamsajili walimsajili lengo lao likiwa kuimarisha eneo la beki wa kati, kilichofanyika ni maamuzi magumu ya kumbadilisha namba kutoka beki wa kati mpka beki wa pembeni jambo ambalo simba wamefanikiwa kwa 100%.Kwasi amekuwa msaada mkubwa wa kuzalisha magoli ya simba kwanza kupelekea mashambuliz katika lango la timu pinzani.

Kwa fikra zangu naona simba ishanufaika na kwasi katika upande wa kushambulia kuliko kuzuia Inaweza kucheza kamari vilevile ya kumrudisha beki wa kati japo tayari inaonekana kuna watu ila inaweza kumrudisha kucheza beki wa kati ili inufaike na kwasi katika kuzuia zaidi hiyo ndio namba asilia ya kwasi Kumrudisha kwasi katikati unaweza kutoa nafasii ya Mohammed Hussein kurudisha makali yake ya msimu uliopita.Nikiamicho ni kwamba kama simba itamchezesha kwasi katikati na wakati huo Mohammed Hussein karudi simba itanufaika na vitu viwili.Kwanza uwezo wa kushambulia utakuwa tofauti wataweza kumtumia kwasi katika mipira iliyokufa ambayo kwasi ameweza kufunga magoli ya kariba hiyo kama manne pia itaweza kujilinda kwani Zimbwe Jr ni mzurii katika kuzuia.

Hadi ilipifika sasa kwasi ametoa somo na atazidi kutoa somo kwa washambuliaji wengine wa VPL.Kwasi mwenye magoli nane hadi sasa ameweza kuwatupa vibaya washambuliaji ambao msimu uliopita walikuwa na magoli mengi.Huwezi kusema kwamba kwasi amebebwa na mfumo wa 3-5-2 ila unaweza kusifu Juhudi zake za kupambana na kutaka kufikia malengo.Kwasi ameweza kuwatupa washambuliaji wengine kama Mbaraka Yusuph,Abdurlahman Mussa,Na wengineo

Kwasi tangu atue katika ardhi ya bongo amekuwa ni mpambanaji haswa,katika msimu wa kwanza akiwa na mbao alionyesha umahiri wa hali ya juu,Na hata alivotimkia lipuli kwasi bado kawa moto wa kuotea mbali.Kwasi anastahili pongezi tena pongezi ya juu kwa beki kuwa na idadi hiyo ya magoli huwezi kusema ni uchawi bali amejituma.

Kwa fikra zangu Mimi kwasi namna anavocheza na jinsi alivo na kiu ya mafanikio msimu huu namtabiria kufikisha idadi ya magoli 10 kama atafikisha zaidi ya hayo 10 ni vizuri ila kwangu Mimi kwa beki akifikisha goli 10 ni kiwango cha hali ya juu sana Naamini washambuliaji butu ( wavunja kuni) somo la kwasi limeeleweka,Zaidi ya hapo kama umeshindwa kuelewa labda ashuke malaika.
Chonde Chonde kwa tuzo ( awards) zile zinazotolewa mwisho ni mwa msimu baada ya kumalizika kwa ligi itakuwa ni ajabu na nitashangaa kama Kwasi atakosa kuambulia tuzo hata moja itakuwa ni maajabu na AIBU
Kwasi RAIA wa Ghana amezaliwa August 13 1995

No comments