EMMANUEL OKWI ATEULIWA KUWA BALOZI
Mchezaji wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi, ameteuliwa kuwa balozi wa Mbeya Tulia Marathon 2018 inayotarajia kufanyika Mei 6, mwaka huu katika viwanja vya Sokoine, jijini Mbeya.
Mbeya Tulia Marathon inaasisiwa na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson na itajumuisha mbio za km 42, km 21, km 150 kukimbia na baiskeli na km 5 kwa vyuo vya ufundi na vyuo vikuu ambapo zitatolewa milioni 40 kwa washindi.
No comments