Breaking News

Kikosi cha Simba Kinachoweza Kuanza dhidi ya Mtibwa Sugar Leo 9.4.2018


Kutokana na Simba Kuwakosa wachezaji wake watatu wa Kikosi cha Kwanza kutokana na kuwa na kadi 3 za Njano kama James Kotei, Juuko Murshid na Erasto Nyoni hiki Ndicho Kikosi ambacho Kinaweza Kuanza siku ya Leo.
KIPA : Aishi Salum Manula naona ataendelea KUWA Numero Uno wa Simba kutokana na Kuwa na Msimu mzuri toka Ligi imeanza akiwa ni moja kati ya makipa waliofungwa magoli machache VPL.
Mabeki wa Pembeni : Namba mbili Nicolas Gyan ambaye amekuwa akiaminiwa siku za Karibuni kucheza kama beki wa Kulia na Namba tatu Asante Kwasi ambaye ameonekana kukosa Mpinzani kama beki wa Kulia
Mabeki wa Kati : Kutokana na Kukosekana kwa mabeki Juuko Murshid na Erasto Nyoni kwenye eneo hili leo msomaji wa Kwataunit Kikosi cha Simba Kinaweza Kushuhudia Salim Mbonde akicheza na Yusuph Mlipili.
Viungo wa Kati : Namba 6 Jonas Mkude bila shaka atarejea katika Kikosi cha Simba baada ya kudaiwa kuwa Fiti kwaajili ya mchezo huu, Huku namba 8 Shomari Kapombe ambaye amekuwa akiaminiwa kwenye mechi za Karibuni bila shaka atacheza katika nafasi hiyo.
>> SOMA HABARI ZETU ZAIDI HAPA <<
Kapombe Licha ya kubadilishiwa namba kutoka namba 2 mpaka Kiungo amekuwa akimudu nafasi hiyo kiasi cha kuibuka kama mchezaji bora wa mechi wa Simba mchezo dhidi ya Njombe Mji.
Winga : Namba Shiza Kichuya anaweza Kuanza kama namba 7 kwenye mchezo wa leo huku Namba 11 Kunaweza kukawa na Option mbili ya Kumtumia Said Ndemla ili aweze kusaidia na eneo la Kati au Kumtumia Haruna Niyonzima ambaye katika mchezo uliopita ALIINGIA Kama Substitution katika mchezo kati ya Simba na Njombe Mji.

Washambuliaji : Kuna mapacha wawili kwenye eneo la ushambuliaji klabu ya Simba Emmanuel Okwi na John Raphael Bocco hawa panga pangua kama wako fiti kwaajili ya mchezo ni lazima wacheze katika mchezo.

No comments