DANTE :TUMECHEZA LIGI KISHUJAA TUMEPITIA CHANGAMOTO NYINGI
Dante amesema kitendo cha wao kufungwa na Tanzania Prisons, mabao 2-0 hakimaanishi mechi tano walizobakiwa nazo watalekeza na amesisitiza wanahitaji kumaliza wakiwa nafasi ya pili.
Beki wa Yanga, Andrew Vecent 'Dante' amesema licha ya kuukosa ubingwa wanahitaji kumaliza michezo yao ilisalia kwa kishindo.
Dante amesema kitendo cha wao kufungwa na Tanzania Prisons, mabao 2-0 hakimaanishi mechi tano walizobakiwa nazo watalekeza na amesisitiza wanahitaji kumaliza wakiwa nafasi ya pili.
"Yanga ni klabu kubwa, kuukosa ubingwa hakumanishi tunashusha hadhi yake bali ni kipindi cha mpito tu na tunachokiangalia ni kupata nafasi ya pili,"amesema Dante mwenye uwezo wa kucheza beki ya kati.
Beki huyo ambaye amekuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Yanga amesema, msimu huu kwao walipambana kishujaa licha ya watu kuwaona wanacheza kichovu na akasisitiza walikutana na changamoto nyingi.
"Ushujaa ni kuonyesha ukomavu wakati wa shida na ndicho tulichokifanya wachezaji wa Yanga na bado tuna malengo ya kuona tumevuna nini mpaka mwisho wa msimu baada ya kumaliza mechi zote," ameongeza.
No comments