Breaking News

KAGAME CUP FAHARI KWA SIMBA NA YANGA

-Michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati (kagame Cup) kutimua vumbi June mwaka huu jijini Dar. Michuano hiyo imekaa miaka 3 bila kufanyika baada ya CECAFA kukosa nchi waandaaji wa michuano hiyo.

Kwa sasa inarudi tena mara ya mwisho michuano hiyo kufanyika ilikuwa mwaka 2015 katika ardhi ya Tanzania ambapo klabu ya Azam Fc walikuwa mabingwa wa kombe hilo. -Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wallece Karia amethibitisha vilabu vya Azam Fc, Yanga Sc na Simba Sc ndio zitashiriki michuano ya Kagame Cup mwaka huu.

Hii michuano zawadi yake mshindi wa kwanza anapata dola Elfu 30 na kombe huku Mshindi wa pili anapata dola elfu 20, na mshindi wa tatu anapata dola Elfu 10. -Achana na hizo milioni 60 kutoka kwa mdhamini wa kagame Cup kwenye mkataba wa Simba na Sportpesa na ule wa Yanga na Sportpesa unajua timu za Simba na Yanga iwapo zitakuwa mabingwa wa kombe la Kagame Cup kwenye mikataba yao watapata bonasi ya milioni 250 kama bingwa wa michuano hiyo.

Vilabu vya Simba na Yanga inatakiwa kuichukulia serious michuano hii timu ikifanikiwa kuwa bingwa atapata zaidi ya milioni 310 kwa mashindano ya wiki tatu si haba hata kidogo ni dau kubwa muno. -Mikataba ya Sportpesa na vilabu vya Simba na Yanga ina bonasi mbalimbali kwa timu hizo kuna bonas iwapo timu itafanya vizuri kwenye michuano inayoandaliwa na shirikisho la soka afrika (CAF) watapata bonasi ya  shilingi milioni 250. -Pia bingwa wa ligi kuu Tanzania bara (vpl)  atapewa milioni 100 kama bonus ya kuwa bingwa wa ligi kuu Tanzania Bara hivyo Bingwa atachukua milioni 180 ikiwa milioni 80 kutoka Vodacom na milioni 100 kutoka Sportpesa. -Kila kheri Simba na Yanga kwenye michuano ya Kagame Cup  

No comments