Breaking News

LICHA YA KUTWAA UBINGWA WACHEZAJI SIMBA WATAKA KUWEKA HISTORIA HII SINGIDA

kama ilivyo kawaida yake kukupatia hatua kwa hatua limeshuhudia nderemo zq wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Mganda Emmanuel Okwi na Nahodha John Bocco bila lumsahau Shizza Kichuya wameonekana kufurahia vilivyo ubingwa huo ambao wameupata kabla ya mchezo wao na Singida United keshokutwa Jumamosi.

Dodoma. Ni nderemo na vifijo usiku wa leo hapa katika hotel ya Golden Crown mahali ambapo Wachezaji wa Simba wameamsha bonge la Sherehe wakishangilia Ubingwa wa Ligi kuu bara ambao umetokana na kupoteza kwa wapinzani wao wakubwa Yanga.
Mwanaspoti kama ilivyo

kawaida yake kukupatia hatua kwa hatua limeshuhudia nderemo za wachezaji wa timu hiyo wakiongozwa na Mganda Emmanuel Okwi na Nahodha John Bocco bila lumsahau Shizza Kichuya wameonekana kufurahia vilivyo ubingwa huo ambao wameupata kabla ya mchezo wao na Singida United keshokutwa Jumamosi.

Licha ya kufanikiwa kuwa mabingwa lakini wachezaji wote wa Simba wameonyesha kuwa na ari kubwa ya kwenda kupambana dhidi ya Singida ili kulinda rekodi yao ya kutopoteza mchezo wowote msimu huu.

No comments