MASHABIKI YANGA WAMJIA JUU KOCHA WAO
Katika hali isiyo ya kawaida mashabiki baadhi wa Yanga wameendelea kusisitiza kutohitaji uwepo wa Kocha wao Msaidizi, Shadrack Nsajigwa katika benchi la ufundi kwa madai ya kuwa ameshindwa kuihimili vizuri.
Timu iYo jana imeenda suluhu ya 0-0 na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mechi hiyo imekuwa ni ya nane kwa mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu Tanzania Bara bila kupata ushindi kufuatia suluhu ya jana.
Ikumbukwe Yanga imetoka kufungwa idadi ya mechi tatu mfululizo katika Ligi Kuu Bara, jambo ambalo mashabiki hao baadhi wameligusia.
Wengi wameeleza kuwa ameshindwa kuisaidia Yanga kutokana na mwendelezo wa matokeo mabovu inayopata hivyo hawaoni faida ya yeye kuendelea kuwa Kocha Msaizidi.

No comments