SIMBA KUITEKA DODOMA MECHI NA DODOMA FC
Dodoma: Mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba watakapomaliza mchezo wao dhidi ya Singida United leo Jumamosi, mapema kesho Jumapili wataanza safari ya kwenda Dodoma kwa ajili ya kucheza mechi maalum wa kirafiki dhidi ya Kombaini ya Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Mabingwa hao, watacheza mechi hiyo itakayohusisha wachezaji wa timu za Dodoma FC na Area C United kwa lengo la kutoa shukrani kwa wapenzi wa timu hiyo baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa.
Kuelekea mchezo huo, Chama cha Soka Dodoma (Dorefa) kimetangaza viingilio vya mchezo huo ambapo mzunguko ni 3000 jukwaa kuu ni 5000.
Namna ya kuingia katika mchezo huo itakuwa ni tofuti kabisa na mechi nyingineziilizopita tiketi zitauzwa getini.
No comments