Breaking News

WAKILI LUGONA AJITOA MAHAKAMANI KUMTETEA HANSPOPPE


Dar es Salaam. Wakili Lugona Mwakipesile amejitokeza jana Jumatatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kesi,  kumtetea Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe.

Mwakipesile anayemtetea Hanspoppe aliyeunganishwa katika kesi ya utakatishaji fedha na kugushi inayowakabili vigogo wa klabu hiyo, amelazimika kujiondoa katika kesi hiyo, baada ya upande wa mashtaka kumtaka amlete mshtakiwa mahakamani.

Hanspoppe na Mfanyabiashara, Franklin Lauwo waliunganishwa katika kesi inayowakabili Rais wa Simba Evance Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu', katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. April 30, 2018, mahakama hiyo iliamuru washtakiwa Hanspoppe na Lauwo wakamatwe popote walipo.

Mahakama hiyo ilitoa amri hiyo baada ya upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Leonard Swai kuieleza kuwa wamewatafuta washtakiwa hao tangu Machi 16 mwaka huu bila mafanikio.

Lakini jana Wakili Mwakipesile alifika mahakamani hapo na kuieleleza mahakama kuwa amefika kumwakilisha Hanspoppe, ambaye yupo nje ya nchi.

Itakumbukwa kuwa, Aprili 30, mwaka huu Mahakama ya Kisutu, ilitoa amri kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe na mwenzake ambaye ni Mfanyabiashara, Franklin Lauwo wakamatwe popote walipo.

Awali, Swai alidai kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa Aveva bado ni mgonjwa ana ameshindwa kufika mahakamani huku mwenzake , Kaburu akiwepo mahakamani hapo.

Baada ya kupitia hoja za pande zote, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 28, mwaka huu ambapo atatoa uamuzi kama mahakama hiyo inauwezo wa kuondoa mshtakiwa wa tatu na wanne katika  kesi hiyo au laa

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka kumi likiwemo la kula njama, matumizi mabaya na kughushi nyaraka ikionyesha Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli.

Pia wanadaiwa Machi 10 na 16, 2016, Aveva na Nyange waliandaa nyaraka za kuhamisha dola za kimarekani 3000,000 kutoka kwenye akaunti ya klabu ya simba kwenda kwenye akaunti ya Aveva wakijua kuwa wanachofanya ni kosa.

No comments