Breaking News

AZAM YAFANYA USAJILI MWINGINE


Klabu ya Azam FC imemsajili Nicolas Wakiro Wadada ambaye alikuwa Nahodha Vipers ya Uganda pia mchezaji wa The Cranes wakati wa michuano ya CHAN.

Wadada ametua Azam ikiwa ni siku kadhaa zimesalia kuelekea michuano ya KAGAME inayotarajia kuanza Juni 28 2018.

Ujio wa beki ni mahususi kwa ajili ya kuboresha nafasi ya ulinzi ya Azam kusaidiana na mabeki wengine akiwemo Aggrey Moris.

Wadada amekuwa mchezaji wanne kusajiliwa kuelekea msimu mpya wa ligi baada ya Donald Ngoma, Tafadzwa Kutinyu na Mudathir Yahya

No comments