Breaking News

GOR MAHIA YAMTOLEA MACHO MSHAMBULIAJI SINGIDA UNITED

Nakuru. Kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr amevutiwa na kiwango cha mshambuliaji Singida United, Danny Lyanga angejua yupo Tanzania angemsajili katika kikosi chake.

Kocha huyo aliyepata mafanikio makubwa nchini Vietnam, alisema Lyanga ni straika mzuri na angeweza kuwaongezea nguvu katika mashindano ya kimataifa.

“Ni mchezaji mzuri, bahati mbaya sikufahamu kama ameondoka Oman, ningemsajili kwenye timu yetu, angekuwa na msaada,” alisema Kerr.
Akimzungumzia straika wake, Meddie Kagere ambaye anahusishwa na timu za Yanga na Azam, Kerr alisema nyota huyo Mnyarwanda amemaliza mkataba, ila bado uongozi haujakaa naye kumpatia mkataba mpya.

Kerr alisema Kagere ni straika mzuri na amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi chake, hivyo kama timu hizo mbili zitampa dau nono huenda akaondoka.

“Yupo mwishoni mwa mkataba wake, anaweza kuondoka endapo watampa ofa kubwa. Ni straika mzuri na amekuwa na kiwango cha kuvutia hapa.”

No comments