Breaking News

KESSY AWEKWA NJIA PANDA YANGA


Licha ya kuonyesha kiwango cha juu kwa msimu mzima, bado mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga hawajafanya mazungumzo na beki wa kulia, Hassani Kessy kuhusu mkataba mpya.


Mkataba wa Kessy na Yanga unamalizika baadaye mwezi huu, baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka miwili na kushinda taji moja la Ligi Kuu.

Kessy ambaye uhamisho wake kutoka Simba kwenda Yanga uligubikwa na matatizo mwaka 2016, amekiri mpaka sasa bado hajajua hatma yake Yanga kuhusu kutia saini mkataba mpya.

“Masuala ya mkataba mpya nimemwachia msimamizi wangu. Mpaka sasa hatujafanya mazungumzo yoyote, nakwenda kupumzika kwanza, siwezi kusema nitaamua nini,” alisema Kessy baada ya Yanga kuondoshwa kwenye michuano ya SportPesa Super Cup mjini hapa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika alisema klabu hiyo itawabakiza nyota wote ambao kocha mkuu, Mwinyi Zahera amependekeza wabaki ingawa aligoma kuwataja majina.

Kessy alijiunga na Yanga Juni 2016. Kabla ya kutua Simba, alikuwa akiitumikia Mtibwa Sugar.

No comments