Breaking News

KIKOSI CHA SIMBA KUONGEZA WAWILI KUONGEZA NGUVU SPORTPESA

Baada ya kufanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Sportpesa Super cup 2018, uongozi wa Simba Sc ya hapa Tanzania umepanga kukiongezea nguvu kikosi chao kwa kuwaongeza wachezaji wawili.

Simba watakutana na Gor Mahia iliyotinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuitoa Singida United kwa jumla ya mabao 2-0, Jumapili ya June 10 mwaka huu Mjini Nakuru nchini Kenya.

Hayo yamefikiwa na uongozi huo uliopo Kenya kupitia kwa kocha Kocha anayekaimu ukocha mkuu kwa sasa Masoud Djuma, baada ya kuuomba uongozi wa klabu hiyo kufanya mpango wa kuwasafirisha hadi Kenya wachezaji wawili ambao ni Mghana Asante Kwasi na Mganda Emmanuel Okwi ili waweze kuongeza msaada kwenye kikosi hicho.

Inaelezwa kuwa Simba wamefikia maamuzi hayo baada baada ya kuona wapinzani wao Gor Mahia kuwa na kikosi kizuri kuliko cha kwao pia sheria za mashindano hayo zinawaruhusu klabu ya Simba kuongeza wachezaji wawili.

Mwanzoni Simba ilikuwa na wachezaji 18 tu baada ya kumwongezea Adam Salamba lakini pia Sheria ya mashindano hayo zinaruhusu klabu kutumia wachezaji 20 hivyo Simba wana nafasi ya kuongeza wachezaji 2, kabla ya kuivaa Gor Mahia katika fainali hiyo ambayo mshindi atajinyakulia kitita cha dola 30,000 na kupata tiketi ya kwenda kucheza na Everton katika uwanja wa Goodison Park nchini Uingereza.

No comments