Breaking News

KOMBE LA DUNIA URUSI SI MCHEZO UJERUMANI YAPIGWA

Moscow, Russia. Bingwa mtetezi wa Kombe la Dunia, Germany imeanza kampeni ya kutetea ubingwa wake vibaya baada a kukubali kutekenywa 1-0 na wabishi wa Mexico, katika mchezo mkali wa Kundi E uliomalizika muda mfupi uliopita katika dimba la Lazhinki.
Vijana wa Joachim Low, waliingia katika mchezo huo wakiwa na rekodi mbaya ambap katika mechi sita za kirafiki walizocheza kuelekea Russia, walishinda mchezo mmoja tu, tangu walipojikatia tiketi ya kucheza kombe la Dunia.
Fomu mbovu ya Germany ilidhihirika mbele ya Mexico, ambayo haikuwa tayari kuwapa nafasi ya kucheza mchezo wao wa kutakata hasa katika eneo la kiungo.
Juhudi za Mexico zililipa katika dakika 35 kipindi kwa goli la pekee na la ushindi lilitiwa kambani na Hirving Lozano, aliyemalizia shambulizi la kushtukiza kW shuti kali lililomzidi kipa Manuel Neuer.
Joshua Kimmich na Timo Werner walikuwa karibu kuipatia Ujerumani bao katika nyakati mbili tofauti lakini walijikuta mashuti yao yakitua katika mikono salama ya Ochoa, ambaye alisimama imara langoni kuhakikisha Wajerumani hao hawafanyi madhara yoyote.
Kipigo hicho kinamuweka Low ba na jeshi lake katika wakati mgumu, wakielekea katika mchezo wa pili, utakaoogwa siku ya Jumapili dhidi ya Sweden, huku Mexico wao wakiisubiri South Korea wakiwa na morali ya kutosha tu.

No comments