Breaking News

MANARA:-SIMBA INALIPA VZUR|KILA MCHEZAJI HUTAMAN KUWA SIMBA|YAMUWINDA FOWARD HATARI


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kuwa kutokana na mabadiliko ambayo Simba imeyafanya, kila mchezaji anatamani kusajiliwa nayo.

Manara amejigamba kwa kusema kuwa katika soka la Tanzania hivi sasa Simba ndiyo timu pekee inayolipa mishahara vizuri na vilevile mchezaji yoyote anatamani kujiunga Simba.

Kiongozi huyo amefunguka wakati akizungumzia mipango yao ya usajili ndani ya klabu ambapo benchi la ufundi limeanza mchakato wa kupata mshambuliaji wa kimataifa.

Tayari Simba wameshaanza kumuwinda mshambuliaji huyo ambaye hajaelezwa atakuwa anatokea nchi ipi huku ukieleza inabidi tusubiri mpaka wakati mwafaka utakapofika.

Wakati Manara akieleza hayo, kikosi cha Simba kimepewa mapumziko ya wiki moja na baada ya kumalizika kitaingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya KAGAME inayoanza Juni 28 2018 jijini Dar es Salaam.

No comments