ALI KIBA AWEKA WAZI KUHUSU MSHAHARA WAKE COASTAL
Ebwana kumbe mkali wa #HitSong KADOGO Ali Kiba halipwi chochote pale Coastal Union…yani maana yake anacheza bureeee!
“Mkataba wangu na Coastal Union mimi silipwi, sichezi kwa pesa nacheza kama burudani kwa sababu napenda mpira na vilevile nimeweza kuitangaza Coastal na Mofaya na kuna vitu tunasaidiana ili kuiendelea Coastal Union ifike mbali zaidi”-Ali Kiba.
“Kiba aliulizwa pia endapo timu kutoka nje zikivutiwa na uwezo wake (kwa mfano KRC Genk) wakataka kumsajili msimamo wake utakuwa upi?
Majibu ya King Kiba: “Mkataba wangu utakuwa uleule, mimi na Mofaya Mofaya na mimi halafu kama kutakuwa na tija mpunga utaongezeka na nitajizatiti zaidi lakini siwezi kuacha muziki, inawezekana vyovyote.”
No comments