Breaking News

HII HAPA SABABU YA BASI LA SIMBA KUPATA AJALI

Mashabiki wa Klabu ya Simba wanaoelekea mjini Kitwe nchini Zambia, wamepata ajali kilomita chache kutoka Mji wa Ndola nchini humo baada ya basi lao hao kugonga lori kwa nyuma.

Imeelezwa kuwa kuna malori mawili yalisimama ghafla bila ya kuweka alama yoyote na kusababisha gari ndogo aina ya Rav 4 ambayo ilikuwa mbele ya basi la mashabiki hao kuyakwepa malori hayo, hali iliyosababisha basi la Simba kuligonga lori mojawapo.

Taarifa zinaeleza kuwa hakuna madhara makubwa isipokuwa mashabiki wachache wamepata michubuko kiasi.

Simba kesho Jumamosi inacheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana FC, mchezo utakaokuwa LIVE KESHO AZAM

1 comment: