KIONGOZI YANGA AMWAGA SIFA NA PONGEZI KWA SIMBA
Aliyewahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro, amemwaga pongezi za dhati kwa Simba baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura ya Algeria katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Muro ameeleza kuwa hatua waliyofikia Simba imewatoa kimasomaso watanzania wote baada ya ushindi huo.
Aidha, Muro amempongeza Msemaji wa Simba, Haji Manara kwa namna anavyojitoa kutia hamasa na morali kwa mashabiki wa Simba na kuwa sababu au chachu ya matokeo mazuri.
Muro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, ameeleza hayo katika ukurasa wake wa Instagram kwa kumwaga pongezi hizo kwa Simba.
"Tuna kila sababu ya kusimama pamoja kama taifa na kuipongeza sana Simba, hakika mmetutoa kimasasomaso watanzania, ndugu yangu Haji Manara hongera, hamasa yako imekuwa chachu ya matokeo mazuri uwanjani. This Is Amazing And Fantastic" - Jerry Muro (Mkuu wa Wilaya ya Arumeru)

No comments