Breaking News

SAPOTI YA MASHABIKI NDIO FURAHA YA KOCHA YANGA



KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema anafurahishwa na sapoti ya mashabiki anayopata akiwa ndani ya Yanga hali inayomfanya afanye kazi kwa juhudi.

Zahera amekuwa kipenzi cha mashabiki pamoja na wachezaji kutokana na namna anavyoibuka kifua mbele kwa kupindua matokeo kila anapozidiwa mbinu.

Zahera amesema mashabiki wa Tanzania ni tofauti na wa nchi ya Congo kwani kule kila ukanda una timu yake tofauti na ilivyo Tanzania.

"Mashabiki wanapenda mpira na wanapenda timu zao, wanazipa sapoti kwa hali na mali hali ambayo inanifanya niwe na furaha kuwa ndani ya Yanga na ardhi ya Tanzania," alisema Zahera.

Matokeo ambayo alifanikiwa kupindua ni pamoja na mchezo kati ya Ndanda ambao alikuwa nyuma kwa bao moja na ule dhidi ya Tanzania Prisons ambao nao alikuwa nyuma kwa bao moja.

No comments