Breaking News

SIMBA HII YAKIMAFIA YATANGULIZA JESHI KUWAPELELEZA AS VITAL


Makachero wa Simba tayari wako DR Congo kuweka mazingira sawa kabla kikosi cha vinara hao wa kundi D michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kuwasili kesho
Simba itaondoka Tanzania Alfajiri ya kesho Alhamisi siku mbili kabla ya mchezo dhidi ya AS Vital utakaopigwa huko Congo
Mmoja wa viongozi waandamizi wa Simba amesema timu hiyo tayari imetanguliza wawakilishi wake Congo ambao watahakikisha hawafanyiwi hujuma ya aina yoyote
Uongozi wa Simba leo unatarajiwa kuweka hadharani msafara wa kikosi chake utakaondoka hapo kesho
Kikosi cha Simba leo kinafanya mazoezi ya mwisho uwanja wa Boko Veterans kabla ya safari hiyo

No comments