Breaking News

VIGOGO WAIPA MTIHANI MZITO SIMBA QUEENS


By Godfrey Godstar,

KOCHA Mkuu wa Simba Queens, Omary Mbweze  amesema kuwa wamepewa kazi ngumu na vigogo wa Simba ili kutimiza lengo la kubeba kombe la Ligi ya Wanawake maarufu kama "Serengeti Lite Women's Premier League' msimu huu.

Kombe hilo lipo mikononi mwa JKT Queens ambao waliwanyoosha Simba kwenye Uwanja wao wa nyumbani Karume kwa bao 1-0 limekuwa likiwapa wakati mgumu makocha wa Simba kubadili mbinu ili kutafuta matokeo.

Mbweze amesema wamekuwa wakitumia nguvu nyingi kuwafundisha wachezaji wao kupata matokeo kutokana na ubora wa kikosi chao walichonacho kwa sasa.

"Tunakazi kubwa ya kufanikiwa kufika malengo ambayo tumejiwekea kwani ushindani kwa sasa wa Ligi ya Wanawake ni mkubwa na kila timu inatafuta matokeo hivyo tutapambana ili kufikia malengo yetu.

"Viongozi wa Simba wanahitaji kuona timu yao inapata matokeo ili kuweza kufungua njia ya kubeba ubingwa kwani ili ufanikiwe kuwa bingwa ni lazima ushinde kwa sasa tupo kamili kwa kila mchezo kuona tunafanya kitu cha kipekee kikubwa sapoti ili tufikie lengo," alisema Mbweze.

Mchezo ujao wa Simba watakuwa ugenini Dodoma kucheza  dhidi ya Baobab wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wao wa hivi karibuni kwa bao 1-0 dhidi ya Mlandizi.

No comments