Breaking News

BEKI SERGIO RAMOS AONYESHA UUGWANA KWA MO SALAH


Beki wa Real Madrid, Sergio Ramos amejutia kitendo cha kumsababishia majeraha ya bega nyota wa Liverpool, Mo Salah na kumtumia ujumbe akimuomba radhi kuwa hakudhamiria kufanya hivyo.

Salah alilazimika kutoka uwanjani kipIndi cha kwanza kwenye mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Liverpool ikitifuana na Real Madrid.

Mchezo huo ambao ulibadilika baada ya Salah kutoka nje, uliisha kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kunyakua taji la ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo na ikiwa ni mara ya 13 katika historia ya mashindano hayo.
Machozi ya Salah yaliwafanya mashabiki waliokuwa uwanjani hapo kushika tama, huku wengine wakishika vichwa kwa hofu majaraha aliyopata huenda yakamsababisha kushindwa kuichezea timu ake ya Misri katika mashidano ya Kombe la Dunia.

Mashabiki wa Liverpool wamemtupia lawama Ramos  kwenye mindano ya kijamii kutokana na kumsababishia majeraha makubwa Salah katika bega.

No comments