Breaking News

MO SALAH ATINGA MADRID AMFUATA RAMOS

England. Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah anapelekwa nchini Hispania kesho Jumatano kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kupata majeraha kwenye bega Jumamosi mwishoni mwa wiki wakati timu yake ilipokutana na Real Madrid kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Shirikisho la Soka la Misri limetangaza kuwa nyota huyo atapelekwa Hispania kwa ajili ya uchunguzi wa kina kutokana na majeraha aliyopata begani.

Hata hivyo, Mo Salah amesisitiza kwamba anatumaini atarejea kwenye hali yake ya kawaida na atakuwa fiti kucheza fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kuanza Juni 14.

Mo Salah anatarajiwa kusafirishwa kesho Jumatano kwenye nchini Hispania.
Mshambuliaji huyo wa Liverpool, alilazimika kutoka nje kwenye fainali hiyo iliyokuwa na ushindani mkali baada ya kupigana vikumbo na beki wa Real Madrid, Sergio Ramos.

Salah aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter juzi Jumapili, akiwathibitishia Wamisri kuwa atakuwepo kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Russia.

Mo Salah anakwenda kutibiwa Hispania ambako  Real Madrid wafalme wa Ligi ya Mabingwa Ulaya 2017/18 wametua nyumbani na taji lao la ubingwa.

No comments