Breaking News

NAHODHA AZAM AFUATA NYAYO ZA BOCCO

NAHODHA wa Azam FC, Himid Mao ameuomba uongozi wa klabu hiyo umuondoe katika kikosi chao kwani anamipango mingine ya kwenda kujaribu bahati katika nchi nyingine kwa lengo la kuendeleza kipaji chake.
Akizungumza Dar es Salaam alisema Afisa Habari  wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga alisema kwa upande wao kama viongozi wamekaa na kukubaliana kuwa ni sahihi kumpa nafasi Himid akajaribu bahati yake.
"Tunaheshimu uwezo wa Himid, lakini kwakua ameomba mwenyewe kuondoka hatuna sababu ya kumlazimisha kuendelea kucheza hapa uongozi umekubaliana na uamuzi wake na tumemruhusu aondoke aende akajaribu huko anakotaka kwenda kucheza," alisema.
Kiungo huyo alishawahi kwenda kufanya majaribio nchi ya Denmark ambapo majaribio yake
yalichukua siku 14 hivyo kutokana na kuaga katika klabu yake inawezekana anaweza akawa anaenda kujaribu bahati yake huko.
Katika hatua nyingine uongozi huo umemalizana na aliyekuwa kocha mkuu wa Singida United, Hans Van Pluijm kwa kumpa mkataba wa mwaka mmoja kwaajili ya kukinoa kikosi chao tayali kwa msimu ujao wa ligi.
Pluijm anajiunga na kikosi hicho akipokea mikoba ya Aristica Cioaba ambaye wameamua kuachana naye kutokana na kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo.
Pia aliongeza kuwa kufuatia dirisha dogo la usajili kuendelea kuwa wazi kwa kuruhusu timu kusajili wao wanaendelea na mawindo kwaajili ya kutafuta wachezaji ambao watakuwa chaguo la mwalimu na kuwaweka hadharani ambapo aliweka wazi kuwa Jumatatu watakuwa na ingizo jipya la mchezaji.

No comments