TETESI ZA SOKA VPL
Baada ya kumnasa Donald Ngoma timu ya azam. Taarifa zinaeleza sasa tayar imewanasa wachezaji wengine wawili safari hii ni Juma Abdur miaka miwili kutoka yanga pamoja na twafadhwa kutinyu miaka miwili kutoka singida.
Mchezaji wa simba shiza ramadhani kichuya ambae apo awali alikuwa anaitajika na Tp mazembe kuna habari za chini kwa Chini zinasema mchezaji huyo atakuwa mali ya azam baada ya mechi ya leo kati ya simba dhidi ya majimaji.
Mchezaji wa simBa Mohammed Ibrahim ajaweka wazi ni wapi Atacheza msimu ujao baada ya msimu huu kumwendea komba ndani ya Club yake ya simba japo taatifa za chini kwa chini zinasema mchezaji huyo ataichezea yanga msimu ujao.
Azam Fc pia wako katika mazungumzo ya mwisho na mshambuliaji wa Mbao Fc mwenye mabao 9 Habib Haji Kiyombo, lakini wanapata upinzani mkubwa kutoka kwa mabingwa wapya wa ligi kuu Bara msimu huu Simba Sc ambao pia wanameonesha nia ya kuhitaji huduma ya nyota huyo kwa msimu ujao wa 2018/19.
Pamoja na kuwa katika hatua hizo Azam Fc pia wako katika hatua za mwisho kumalizana na kiungo mshambuliaji wa Simba Shiza Ramadhan Kichuya, dili hili linaweza kukamilika baada ya mechi ya leo dhidi Majimaji Fc
No comments