Breaking News

HABARI MPYA NA NZURI KWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA LEO KUELEKEA SPORTPESA

Baada ya kupeleka kikosi cha wachezaji 18 katika mashindano ya Sportpesa Super Cup klabu ya Simba inatarajiwa kukiongezea nguvu kikosi hicho leo Jumamosi.

Simba inatajiwa kuwaongeza washambuliaji watatu katika michuano hiyo ambao ni Nahodha John Bocco, wapya wawili ambao ni Adam Salamba na Mohamed Rashid ‘Mo’ ambao wanatarajiwa kuondoka leo kuelekea Kenya kwa ajili ya michuano hiyo itakayokuwa Live kupitia channel ya Start TV ya jijini Mwanza.

Simba watafungua mshindano hayo na klabu ya Kariobangi ya huko Kenya ya Charks Jumatatu ya June 04.

Pia uongozi w Simba ulithibitisha kuwa mshambuliaji wao Kinara wa mabao msimu ulioisha Mganda Emmanuel Okwi na Juuko Mrishid waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa hao wataungana na timu huko huko Kenya wakitoa Uganda.

Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kesho Jumapili ya June 03 hadi June 10 inashirikisha timu jumla ya klabu 8 huku 4 zikiwa z Kenya na 4 za Tanzania.

No comments