Breaking News

MTIBWA DHIDI YA SINGIDA MOTO KUWA LEO NDANI YA ARUSHA

Arusha: Mtibwa Sugar na Singida United zitaonyesha kazi katika  fainali ya mashindano ya Kombe la FA utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo saa 10:00 jioni.
Hii ni mara ya kwanza kwa jiji la Arusha kuwa wenyeji wa fainali za michuano mikubwa kwa miaka ya hivi karibuni hivyo inavutia watazamaji wengi pamoja na viongozi tofauti wa soka na serikali.

Nahodha wa Singida United, Nizar Khalfan alisema wametinga hatua hiyo sio kwa kubahatisha na wanalenga kuwakilisha Taifa katika mashindano ya kimataifa tofauti watu wanavyowazungumzia.
Naye nahodha wa Mtibwa Sugar, Shabaan Nditi alisema watakachokifanya katika mchezo huo ni maandalizi ya muda mrefu waliyojiandaa chini ya kocha wao Zuberi Katwira.

“Singida ni timu yenye wachezaji wengi wa kigeni na wana kocha mwenye uwezo mkubwa lakini Mtibwa ni timu imejaa wachezaji wazawa wenye vipaji vya namna yake”

Makocha wa pande zote mbili wametamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo huku Kocha wa Singida, Hans Van De Pluijm akieleza kuwa anataka kuondoka kwenye kikosi hicho kwa kuwaachia heshima watu wa Singida.
“Nimewasili na kikosi kizima mkoani hapa hivyo yoyote kati yao anaweza akacheza ndio maana sijataja kikosi kitakachocheza kwani binadamu anaweza kubadilika muda wowote hivyo ripoti ya daktari ya asubuhi ndio itanipa fulsa ya kuweka bayana kikosi kitakaochoza”
Naye Zuberi Katwira amewasifu wachezaji wake huku akieleza kuwa wengi wanazungumzia adhabu yao kuwa ndio itawafanya kutoka kwenye mstari jambo ambalo alisema siyo sahihi kulizungumzia.

VIINGILIO VYA MCHEZO

TFF ilimetangaza kiwango cha chini katika mchezo huo Sh 1,000 kwa jukwaa C’ 2000 jukwaa B’ na jukwaa kuu ambalo haliingizi watazamaji wasiozidi 500 litakuwa 10,000 katika uwanja huo unaoingiza watazamaji 11,000 kwa mujibu wa viongozi wa chama cha soka Mkoani hapa (ARFA).

Tiketi za mcheo huo zitaanza kuuzwa asubuhi katika mageti ya uwanja huo huku milango itakuwa tayari kufunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi kabla ya wageni rasmi kuwasili uwanjani hapo.

TFF YATOA NENO

Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Nchini (TFF) Wilfred Kidao alisema kuwa suala la linalowakabili Mtibwa linazungumzwa tofauti kwani adhabu yao ilionesha miaka mitatu pamoja na kulipa fedha taslimu lakini haikusema miaka mitatu wanapokuwa mabingwa.

“Tumewasilia na CAF ili kujua ufafanuzi zaidi ya jambo hilo hivyo sioni sababu ya kuendelea kulikazia kwani majibu yake yapo wazi na tutaendelea kulifafanua kila linapohitajika.
Mwamuzi Emanuel Mwandembwa (Mwanza) amepewa jukumu la kusimama katikati kwenye mchezo huo akisaidiana na Mohamed Mkono (Tanga), Ferdinand Chacha (Mwanza) pamoja na Jonesia Rukiya (Kagera).

No comments