Breaking News

OKWI BOCCO WAMJAZA MO

NYOTA mpya wa Simba, Mohammed ‘MO’ Rashid, kumbe hajatua Msimbazi kizembe, kwani anaujua fika uwezo walio nao John Bocco na Emmanuel Okwi na tayari ameanza kujipanga ili kuhakikisha hachomeshwi mahindi na mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara.

Straika huyo anayetokea Prisons, ameliambia Mwanaspoti hajasaini Simba ilimradi, bali ametua akiwa na mipango yake kichwani, akihitaji kucheza na kiwango chake kilekile na zaidi ili afike mbali, hivyo uwepo wa Okwi na Bocco kwake utamsaidia kujituma zaidi.
“Bocco na Okwi mnaowaona leo haina maana kwamba walianza kwa kasi hiyo hiyo, naamini wametoka mbali ila walijitambua. Mchezaji mzuri ni yule ambaye haogopi changamoto, badala yake anazikabili,” alisema. “Naheshimu uwezo wao ila watanifanya nisibweteke na kujua nina kazi ngumu Simba, nafurahia uwezo wao na nipo tayari kuonyesha kwamba sikuja kushanga mjini bali kufanya kazi.”

Awali mchezaji huyo aliwahi kuhusishwa na Yanga, ila Simba iliwazidi kete watani zao na kumsainisha mkataba wa miaka miwili.

No comments