Breaking News

UONGOZI SINGIDA WAMKINGIA KIFUA BEKI HUYU




Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga amelaani kitendo cha uongozi wa Yanga kusema beki waliopewa hakuwa na kiwango cha kuichezea Yanga.

Beki, Elisha Mloiwa raia wa Zimbabwe alitua Yanga na wao waliamua kumuacha baada ya kumsajili Yondani saa nne usiku.

“Mloiwa ni mchezaji mwenye kiwango kizuri, alicheza Afcon. Vipi unasema hana kucheza Yanga, hii dharau inatokea wapi, hili si jambo zuri,” alisema.

Sanga amesisitiza kwamba mchezaji huyo ataitumikia Singida United na anaamini atawaonyesha Yanga kiwango chake.

Ameendelea kusisitiza kawa kwamba viongozi wa Yanga wanataka kuwadanganya wanachama wao

No comments