Breaking News

HAZARD KUIKACHA CHELSEA?

Siku zinahesabika kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili la mwezi January kwa klabu mbalimbali Ulaya, hivyo sio jambo la ajabu sana kusikia mchezaji flani akitangazwa kuhusishwa kwenda katika timu Fulani, kwa upande wa Chelsea wanaweza kupata pigo kwa kuondokewa na mchezaji wao tegemeo raia wa Ubelgiji Eden Hazard.
Eden Hazard amerudia kauli yake ambayo inawaumiza mashabiki wengi wa Chelsea kwa sasa kuwa ana uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo, Chelsea tayari wamemalizana na Ngolo Kante kwa kumuongezea mkataba mrefu na sasa wanapambana kuhakikisha Hazard anasalia katika kikosi cha Maurizio Sarri. “Kwa sasa nabakia Chelsea nina mkataba hadi mwezi Juni mwakani kama sitaongeza mkataba basi kuna uwezekano wa kuondoka lakini sioni nikiondoka Chelsea mwezi Januari, nisingependa kufanya hivyo kwa klabu na mashabiki lakini katika kipindi cha usajili cha majira ya joto naona uwezekano wa mimi kuondoka lakini pia inawezekana nikamalizia soka Chelsea” alisema Hazard akihojiwa na Canal Plus
Hadi sasa Eden Hazard amedumu na Chelsea kwa miaka sita toka alipojiunga na timu hiyo mwaka 2012 akitokea klabu ya Lille ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa pound milioni 32, kwa miezi kadhaa sasa Hazard amekuwa akihusishwa kuhitajika na Real Madrid licha yay eye kukiri kuhitaji kwenda kucheza soka Hispania.

No comments