HIZI HAPA HESABU ZA SIMBA KWA NKANA
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na wawakilishi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Simba, wameanza kujiandaa kwa ajili ya kuwavaa Nkana FC katika mchezo wa hatua ya kwanza utakaopigwa Desemba 14 Zambia.
Simba wameanza mazoezi leo katika uwanja wa Boko wakiwa chini ya kocha mkuu raia wa Ubelgij Patrick Aussems ambaye hesabu zake kubwa ni kupata ushindi wa mapema.
Aussems amesema kuna kazi kubwa kupata ushindi ila inawezekana kwani hicho ni kipambele namba moja kwa wachezaji wake na timu kiujumla.
"Tunatambua tuna kazi ngumu ya kufanya ili kupata matokeo hilo lipo wazi ila imani yetu tutafanikiwa kushinda ili kusonga mbele, mbinu mpya na kujiamini kwa wachezaji wangu kunanipa furaha," alisema.
Simba walifanikiwa kutinga hatua hiyo baada ya kuifunga mabao 8-1 Mbabane Swallows ambapo mchezo wa nyumbani walishinda mabao 4-1 na marudiano nchini Eswatini walishinda mabao 4-0 huku Nkana FC ya Hassan Kessy wana jumla ya mabao 3-1 walicheza dhidi ya UD Songo
No comments