KING AWEKA HISIA ZAKE KURIDHI MIKOPA YA MASOUD DJUMA SIMBASC
Dar es Salaam. Kocha wa zamani Simba, Abdallah 'King' Kibadeni ameweka wazi hisia zake akisisitiza kuwa bado anatamani kurudi kukinoa kikosi hicho cha mabingwa wa Ligi Kuu.
Kibaden ametoa kauli hiyo wakati Simba ikiwa haina kocha msaidizi tangu alipoondoka, Masoud Djuma miezi minne iliyopita.
"Napenda kurudi kufundisha Simba, ikishindikana kwenye ukocha basi niwe mshauri wa timu," alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba.
Kibaden aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu hiyo alisema ameiangalia Simba kwa muda mrefu na kubaini inahitaji kuwa na mtu ambaye atamsaidia kocha mkuu, Patrick Aussems.
"Unajua hata busara kwenye mpira uwa inahitajika, kocha anahitaji mtu mzawa wa kumshauri na kushirikiana naye, naamini mtu sahihi ni mimi, naipenda Simba na ninatamani kurudisha uzoefu wangu wa mpira kwa mara nyingine kwenye timu hiyo," alisema Kibadeni.
Alisema walipofikia Simba sasa wanahitaji kuwa na watu sahihi wa kumshauri na kushirikiana na kocha, hivyo anaamini yeye Kibadeni ataitendea haki kama atapewa nafasi hiyo.
Kocha huyo ameondoka Simba akiwa na kumbukumbu ya sare ya mabao 3-3 dhidi ya Yanga akiwa ndiye kocha mkuu wa timu hiyo iliyoanza kufungwa mabao 3-0 dakika 45 za kwanza na Simba kutoka nyuma na kusawazisha mabao yote kipindi cha pili.
Mbali na ukocha, Kibadeni ana rekodi ya kufunga mabao matatu 'hat trick' kwenye mechi ya watani Simba na Yanga, rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa na mchezaji mwingine katika mechi ya watani hao kwa zaidi ya miaka 30.

No comments