Breaking News

KIUNGO YANGA AAMUA KUBWAGA MANYANGA






Kiungo wa klabu ya Yanga, Mzibambwe, Thaban Kamusoko, ameamua kuchana rasmi na mabingwa hao wa kihistoria.

Kamusoko kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika akiwashukuru wadau na mashabiki wa timu hiyo kwa muda wote aliokaa na timu.

"Katika kukaa kwangu hapa Yanga, nimejifunza vitu vingi , nilikuja Yanga na nilijifunza vile watu wanathamini pale unapoonesha kujitolea katika timu. 

Ninataka kusema Ahsante kwa mashabiki wote kwa mapenzi mliyonipa na mapenzi ambayo bado mnanipa. Ninathamini sana.

Ahsante kwa mara nyingine tena “ - Ameandika kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko katika Instagram yake" ameandika.




No comments