KOCHA MKUU YANGA AIPA SIMBA MBINU ZA KIKATILI KUIUA AS VITAL
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amewaoa mbinu nzuri Simba ya kupenya katika hatua ya makundi kuelekea robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Zahera ambaye yuko mjini Shinyanga kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui, amewataka Simba kucheza mchezo wa kufunguka ili kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya AS Vita.
Kauli ya Zahera imekuja kufuatia Simba ambayo inaiwakilisha nchi, itakuwa na kibarua cha mechi hiyo kubwa kesho Jumamosi huko Kinshasa, Congo.
Zahera amewaasa Simba kutocheza kwa lengo la kusaka alama moja pekee ili waje kupambana kupata matokeo nyumbani Tanzania akiamini inaweza ikawa jambo gumu kwao.
"Simba wanapaswa kucheza kwa kufunguka, nimesikia kuwa wameenda na malengo ya kusaka alama moja pekee, si vema wakafanya hivyo maana inaweza ikawagharimu hapo baadaye, watafute ushindi na si alama moja" alisema.
Tayari kikosi cha Simba kimeshawasili jijini Kinshasa jana na kilifanya mazoezi siku hiyohiyo tayari kujiweka sawa kuelekea kipute hicho.
No comments