MADRID SASA YAAMUA KUVUNJA BENKI TAYARI KUMNYAKA MBADALA WA CR7
Real Madrid ina matumaini ya kumsaini mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard kwa chini ya kitita cha yuro 100m {£88m) kilichowekwa na Chelsea kwa klabu yoyote inayomuhitaji mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye kandarasi yake inakamilika mwezi Juni 2020. (marca)
Kinda wa Chelsea na Uingereza anayeichezea timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 19 Callum Hudson-Odoi yuko tayari kukataa ofa ya kandarasi yenye thamani ya £85,000 kwa wiki na kuhamia katika klabu ya Bayern Munich nchini Ujerumani kwa kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 anasema ana fursa nyingi za kujiimarisha katika ligi hiyo ya Bundesliga.. (Mail on Sunday)
Arsenal inataka winga wake za wazamani Marc Overmars kuwa mkurugenzi wa kiufundi katika uwanja wa Emirates kwa kuwa mkufunzi Unai Emery na kiongozi wa usajili wa wachezaji Seven Mslintat hawawezi kushirikiana.
Mchezaji huyo wa zamani wa Uholanzi , Overmars mwenye umri wa miaka 45 ni mkurugenzi wa klabu ya Uholanzi ya Ajax. (Sunday Mirror).
Hatua ya mshambuliaji wa West Ham Marco Arnautovic ya kujiunga na klabu ya Guangzhou Evergrande nchini China imetibuka baada ya klabu hiyo kujiundoa katika makubaliano hayo ya £45m kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 (Mail on Sunday).
Chelsea imewauliza mabingwa wa la Liga Barcelona kuhusu kumnunua mchezaji wao anayedaiwa kuwa na thamani ya £100m kutoka Brazil Philippe Coutinho, 26. (Sunday Express).
Uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain kuelekea Chelsea utamweka raia huyo wa Argentina kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa kitita kikubwa katika klabu hiyo cha £270,000 kwa wiki.
Manchester City huenda ikamnunua kwa mkopo kiungo wa kati wa Schalke Sebastian Rudy ,28, (Sun on Sunday).
Mchezaji wa zamani wa Man United Paul Scholes anatarajiwa kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya Oldham (telegraph).
Mhambuliaji wa Stoke na Uhispania Bojan Krkic, 28, ameanza mazungumzo ya kutaka kuhamia katika ligi ya Marekani ya MLS ambapo atajiunga na klabu ya New England Revolution, ambayo hufunzwa na aliyekuwa kocha wa Blackburn Brad Friedel. (Sun on Sunday).
Mshambuliaji wa Paris St Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 20, anasema kuwa huenda akavutiwa na uhamisho wa kuelekea Real Madrid katika siku za usoni. (AS)
Mkufunzi wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa klabu hiyo huenda ikampata mchezaji atakayeziba pengo lililowachwa na mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane katika taasisi yake ya mafunzo ya soka kupitia dirisha la uhamisho. (London Evening Standard)
Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery anatumaini ya kufanya usajili wiki hii huku kukiwa na ripoti zinazomuhusisha kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suare 25. (Daily Star Sunday).
Philippe Coutinho alihamia Barcelona kutoka Liverpool
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amefutilia mbali uwezekano wa Philippe Coutinho, kurejea Liverpool mwaka mmoja baada ya kumuuza kwa Barcelona kwa pauni milioni 142. (Liverpool Echo)
Liverpool wameweka dau la pauni milioni 61 kumnunua mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 19, kutoka Benfica. (Correio da Manha - in Portuguese)
Meneja wa Monaco Thierry Henry anataka kumsajili kwa mkopo kiungo wa kati wa Manchester United mbelgiji Marouane Fellaini, 31. (RMC - in French)
Mshambuliaji wa Juventus na Argentina Gonzalo Higuain, 31, yuko mjini London kutia saini mkataba wa kujiunga na Chelsea ili aweze kushiriki mechi ya kombe la Carabao Alhamisi ijayo dhidi ya Tottenham. (Sun)
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri anapania kuimarisha kikosi chake kwa kumsaini kiungo mwingine wa kati kabla dirisha la uhamisho wa wachezaji kufungwa. (Guardian)
Bayern Munich wamemkabidhi Chelsea winga Callum Hudson-Odoi kwa kadarasi ya pauni 85,000 kwa wiki. (Sun)
No comments