MCHEZAJI YANGA AIKOSOA LIGI KUU BARA, ASEMA HAINA MVUTO KWA SASA
Mchezaji wa zamani wa Yanga, Edibily Jonas Lunyamila, amesema kuwa ligi imepoteza mvuto kwasababu ya kuwa na viporo.
Amegusia kwa kuwataja Simba kuwa wna mechi za viporo nyingi japo akikiri kuwa ni kweli wanashiriki mashindano ya kimataifa na hakuna namna au haja ya kuwalaumu.
Lunyamila ameeleza kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa kujipanga namna ya kuifanya ligi iwe na ubora, walau kama ni viporo viwe viwili au vitatu.
"Unajua ligi yetu ni nzuri lakini kwa msimu huu imekuwa haina mvuto zaidi haswa kutokana na uwepo wa viporo vingi ambavyo vinapunguza ladha.
"Ingefikia hatua walau kuwe na viporo viwili ili kuifanya ligi iende sawa, sasa unakuta timu moja ina mechi nyingi, hili linasababisha kupotea kwa utamu wa ligi" alisema.
No comments