Breaking News

MSAFARA WA WACHEZAJI 20 WA SIMBA SC KUTUA CONGO

Msafara wa wachezaji 20 wa Klabu ya Simba ukiambatana na benchi la ufundi pamoja na baadhi ya viongozi utaondoka nchini kesho Alhamis Januari 17, 2019 kwenda Kinshasa nchini DR Congo kuwakabili AS Vita katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kuwa msafara huo utaondoka saa 2 asubuhi kupitia Nairobi na kisha kuunganisha hadi Kinshasa na utarejea nchini siku ya Jumapili usiku.

Mchezo huo ni wa pili kwa Simba kwenye hatua hiyo na unatarajiwa kuchezwa Jumamosi Januari 19, 2019 saa 11:00 jioni za DR Congo sawa na saa 1:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na utakuwa LIVE AZAM

No comments