Breaking News

PIGA HILI LA NYONI SIMBA NI MAUMIVU


Beki Erasto Nyoni atakaa nje kwa wiki tatu akiuguza majeraha ya goti.

Nyoni aliumia wakati Simba ikiivaa KMKM katika mechi ya Kombe la Mapinduzi, jana.

Kutokana na maumivu, jana Nyoni alikimbizwa hospitali wakati mechi ikiendelea.

Awali Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema alikuwa ameona jeraha si kubwa sana ingawa ilitakiwa kufanya vipimo kwanza.

Nyoni ambaye alijiunga na Simba akitokea Azam FC amekuwa sehemu ya nguzo ya ulinzi katika kikosi cha Simba ambacho kimefuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi

No comments