Breaking News

YANGA YAANZA NA USHINDI MAPINDUZI


Kikosi cha Yanga kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KVZ ya Zanzibar katika michuano ya Mapinduzi CUP.

Bao pekee la Yanga limewekwa kimiani na Shaban Mohammed mnamo dakika ya 76 ya mchezo.

Yanga ambayo imetumia asilimia kubwa ya kikosi cha vijana, ilionesha mpira wa kiufundi na wa kuwapa wakati mgumu wenyeji wa mashindano hayo.

Kwa ushindi huo Yanga inaweka alama zake tatu mkononi katika mechi ya kwanza msimu huu kwenye mashindano hayo.

Kesho watani zao wa jadi, Simba wataanza kibarua chao dhidi ya Chipukizi FC, majira ya saa 2 na dakika 15 za usiku.

No comments