YASHUSHWA HADI DARAJA LA NNE
Timu ya Madini FC ya mkoani Arusha (pichani) imeshushwa daraja hadi Ligi Daraja la Nne ngazi ya Wilaya kutoka Ligi Daraja la Pili baada ya kutofika kwenye mchezo wake dhidi ya Milambo ya Tabora.
Mbali na kushushwa madaraja hayo mawili, timu hiyo pia imepigwa faini ya shilingi milioni 2, adhabu zote zikiwa ni kwa mujibu wa kanuni ya 28 ya Ligi Daraja la Pili kuhusu timu kutofika uwanjani.
Kwa mujibu wa bodi ya ligi ambayo imetangaza adhabu hizo leo, matokeo ya mechi zote ilizocheza timu hiyo yamefutwa ili kutoa uwiano sahihi kwa timu zilizobaki.

No comments