ZAHERA AMTAJA MMOJA PEKEE YANGA ANAYEAMINI ATAIPELEKA STARS AFCON BILA KIZUIZI
Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera, amesema Taifa Stars haina sababu ya kushindwa kufuzu kuelekea AFCON 2019 sababu ina wachezaji nyota.
Zahera ambaye amekuwa akiviteka vichwa vya habari kila wiki amefunguka kwa kueleza ni lazima Stars ipate nafasi hiyo na itashiriki mashindano hayo makubwa.
Kocha huyo amemtaja mchezaji wake Ibrahim Ajibu kuwa ni fundi wa kipee kwake na akimpa nafasi ya kuipa nguvu Stars katika mashindano hayo.
Amemuelezea Ajibu kuwa ni fundi kulingana na namna ambavyo ameisaidia Yanga mpaka sasa kuendelea kuwa juu ya Simba na Azam katika msimamo wa ligi.
Aidha, Zahera amesema kuwa Uganda The Cranes ambayo itakuja kucheza hapa nchini hapo baadaye ni lazima ipoteze kwakuwa Stars ina wachezaji wenye vipaji.
Ameeleza Uganda haitaweza kuwa na ubavu wa kuifunga Stars hivyo uwezekano wa kufuzu kwenda AFCON utasalia hapahapa Tanzania.
No comments