Breaking News

HUKO YANGA MAMBO NI MOTO, LWANDAMINA AZUILIWA

Wachezaji wa Zesco ya Zambia juzi usiku walikuwa wakishangilia baada ya kuelezwa na mabosi wao kwamba, kocha wao wa zamani Lwandamina anarejea kufundisha tena kikosi hicho.
Baadhi ya wachezaji wakavujisha taarifa hizo kwa mashabiki na ghafla shangwe zikashika kasi huko mitaani, lakini amesikia hizo taarifa na amefunguka machache sana.
Lwandamina ameliambia Mwanaspoti jana kuwa, bado yuko Yanga na hajutii kuwepo kwake kwa kuwa uamuzi wake. Kibarua cha kocha wa Zesco kipo wazi baada ya aliyekuwepo kubwaga manyanga juzi baada ya matokeo mabovu ya timu yake.
Hata hivyo, Lwandamina amsema kule Zambia karibu nusu ya klabu zinataka huduma yake kutokana na rekodi zake bora, lakini hajafikiria kuiacha Yanga na akili yake ni kushinda mataji na kutamba kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
“Nimesikia hizo taarifa (Anacheka) hakuna ukweli kuwa naondoka hapa kama ingekuwa hivyo ningefanya muda mrefu sana ila nimeamua kubaki Yanga kwa maamuzi yangu.
“Zambia kila wakati napokea ofa za timu kuhitaji nikafanye kazi na nina ofa nyingi sana, lakini ukweli bado nipo Yanga natumikia mkataba wangu,î alisema. HUKO YANGA MAMBO NI MOTO, LWANDAMINA AZUILIWA

No comments