KAGERA SUGAR SAWA NA CHELSEA
Baada ya Kagera Sugar kulazimishwa sare ya 1-1 na Ndanda kwenye mchezo ligi, kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime amesema kufanya vibaya kwa timu hake msimu huu ni moja ya matokeo ya mchezo wa soka.
Maxime amefananisha matokeo ya timu yake na Chelsea ambayo ilibeba ubingwa wa EPL msimu uliopita lakini msimu huu imekuwa haifanyi vizuri. Chelsea ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 57 baada ya kucheza mechi 32
“Unaweza kuwa na timu nzuri lakini usifanye vizuri, Chelsea msimu uliopita ilichukua ubingwa wa England, utasema sasa hivi wana kikosi kibaya? Kuondoka kwa Diego Costa ndio kuyumba kwa Chelsea? Ni matokeo tu ya mpira”-Mecky Maxime, kocha Kagera Sugar.
Msimu uliopita Kagera Sugar ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi huku Maxime akishinda tuzo ya kocha bora wa msimu.
No comments