MANCHESTER CITY YALITAKA TAJI HILI
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ameweka wazi kuwa klabu hiyo inahitaji taji la Ulaya kutokana na uwekezaji ambao umefanyika katika kipindi cha mika 10 na tayari umeleta mafanikio kwenye ligi ya ndani.
"Tunahitaji mataji ya Ulaya japo ni jambo gumu lakini tunalitarajia iwe msimu huu au msimu ujao lakini mapema tu tunahitaji kutwaa taji hilo'', amesema Guardiola kwenye mkutano na wanahabari kuelekea mchezo wa marudiano kesho dhidi ya Liverpool.
Akiongelea kuhusu uwezekano wa kupindua matokeo ya mechi ya kwanza ambapo walipoteza kwa mabao 3-0 ugenini, Pep amesema kila kitu kinawezakana ndio akitumia mfano wa walichofanya Barcelona msimu uliopita walipopindua 4-0 na kushinda 6-1 dhidi ya PSG.
Aidha Guardiola amesema kuwa najua wazi timu yake inahukumiwa kwa matokeo ya hivi karibuni lakini yeye kama kocha ana furaha na kiwango cha timu yake na anaamini kuwa ndio timu yenye kiwango kizuri kwasasa.
Manchester City leo watakuwa wenyeji wa Liverpool kwenye mchezo wa marejeano kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo matajiri hao wanahitaji kushinda kuanzia mabao 4 huku wakiwa hawajaruhusu wavu wao kuguswa ili kuweza kupata nafasi ya kucheza hatua ya nusu fainali...
No comments