Breaking News

KAMUSOKO KAMTAJA MCHEZAJI ANAYE TAMANI KUCHEZA NAYE KATIKA KIKOSI CHA YANGA

KIUNGO wa Yanga, Thaban Kamusoko ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeruhi ya goti, amerejea kikosi kusaidia akianzia na mechi dhidi ya Kagera Sugar, lakini kuna kitu amekimiss sana uwanjani.
Kamusoko, ambaye alionekana kutokuwa fiti katika kiwango chake kilichozoeleka, amewatoa hofu mashabiki wa Yanga akisema amerejea na yuko fiti kwa mapambano.
“Natamani kucheza wakati mmoja nikiwa na Papy Kabamba kwa kuwa, jamaa yuko vizuri na amekuja kuongeza nguvu kikosini.
“Niwatoe hofu mashabiki wa Yanga dhidi yangu, nimerudi na karibuni kiwango changu kitarajea kwenye nafasi yake. Nafanya mazoezi ya kutosha ili kujiweka fiti zaidi,” alisema Kamusoko.

No comments