MWENYEKITI WA KAMATI YA MASHINDANO HUSSEIN NYIKA KAAMUA KUTOA SHUKRANI ZAKE KWA MASHABIKI WA YANGA
Mwenyekiti wa kamati ya Mashindano ya Yanga Hussein Nyika amewashukuru mashabiki kwa sapoti kubwa waliyoonyesha kwenye mchezo wa jana dhidi ya Wolaitta Dicha.
Uhamasishaji uliofanywa kupitia vyombo vya habari na makundi ya mitandao ya kijamii ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani mashabiki wengi walijitokeza uwanja wa Taifa kuipa sapoti Yanga iliyoanza vyema kwa ushindi wa mabao 2-0.
"Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano HUSSEIN NYIKA anawashukuru,wanachama,mashabiki na wapenzi wa Yanga sc kwa mchango wao mkubwa katika kufanikisha ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya WD SC," imesomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga.
Tayari maandalizi ya mchezo ya marudiano utakaopigwa April 18 nchini Ethiopia yameanza na mashabiki wanaotaka kwenda kuushuhudia mchezo huo watalipa kiasi cha Dola 350 tu.
No comments