KISA PESA YANGA YAAMUA KUFANYA KIMYAKIMYA
Yanga wameamua kufanya usajili wao kwa uficho kwa hofu ya kupokonywa tonge mdomoni na wapinzani wao ambao wanaonekana kuwa wako vizuri kifedha.
Mmoja wa wajumbe wa kamati maalum ya Yanga, ameaimbia SALEHJEMBE kwamba wamekuwa wakifanya mambo yao kimya kutokana na hofu ya kuwaingiza inaowataka katika vita ya kuwaniwa na Simba au Azam FC.
"Sisi hatuko vizuri sana kifedha ndugu yangu, tunachofanya ni kutafuta wachezaji kwa ushauri wa wataalamu na hasa makocha na kuangalia mapendekezo sahihi.
"Baada ya hapo, usajili wetu unakuwa wa kimyakimya sana. Unajua wenzetu wakisikia mchezaji anatakiwa Yanga hata kama hawamtaki, basi wanamsajili tu, sijui ni kukomoana," alifafanua.
Hadi sasa Yanga bado haijafanya usajili unaoeleweka na imekuwa ikielezwa suala la ukata wa kifedha limekuwa tatizo kuu linalowatatiza.

No comments