BAADA YA KUVUNJA REKODI YA MSUVA OKWI AIFIKIA REKODI HII
Hapo jana katika ligi kuu yaTanzania Bara timu ya soka ya Simba Sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Magoli ya ushindi huo yalifungwa na na nahodha wao John Bocco dakika ya 35 na Emmanuel Okwi dakika ya 80 kwa mkwaju wa penati baada ya Bocco kuchezewa faulo.
Ushindi huo unaendelea kuiweka Simba kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Tanzania Bara dhidi ya Yanga kwa tofauti ya point 11 dhidi ya Yanga wanaowafuatia kwa kuwa na jumla ya point 47 ila Simba ikiwa mbele ya Yanga kwa michezo miwili.
Goli alilofunga Okwi kwenye mchezo huo linamfanya kufikisha jumla ya magoli 19 ya ligi kuu msimu huu
Baada ya kuvunja rekodi ya Msuva na Abdulhaman Mussa ya msimu uliopita, Emmanuel Okwi anakuwa amefikia rekodi ya John Bocco aliyoiweka akiwa Azam FC na Amissi Tambwe ya kufunga magoli 19 kwa msimu lakini Okiwi ana nafasi ya kuvunja rekodi hiyo kwani zimebakia game sita VPL kumalizika.......
No comments