Breaking News

MWALI WA MABINGWA SIMBASC ATUA TAIFA MPYA KABISAA

Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambalo Klabu ya Simba watakabidhiwa leo Jumamosi na Rais John Magufuli, limewasili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kombe hilo ambalo jipya kabisa litakuwa ni la 19 kwa Simba lakini hili sasa ni la kihistoria kutokana na matukio hayo.

Kombe hilo lenye rangi ya dhahabu pamoja na medali limeletwa uwanjani hapa na maafisa wa Vodacom ambao ndiyo wadhamini wa Ligi Kuu.
Magufuli atakabidhi kombe hilo leo, lakini haijajulikana kabla au baada ya mchezo.

No comments