FAHAMU KUHUSU,Real Madrid na El Clasico yako hapa
Sasa ni hivi, kama ulikuwa hujui ni kwamba tangu kuanzishwa kwa La Liga hii itakuwa mechi ya 176 kwa timu hizi kukutana katika michuano hii ya Hispania lakini kiujumla kabisa hii itakuwa El Clasico ya 237.
Katika michezo 175 ambayo tayari Barcelona na Real Madrid wamekutana, vijana wa Zinedine Zidane wanaongoza kwa kuiburuza Barcelona, hadi sasa Real Madrid wameshinda mara 72, suluhu mara 70(tofauti ikiwa mbili tu) na mara 33 suluhu.
Lakini rekodi zinaonesha kwamba utawala wa Real Madrid kwa Barcelona ulimalizwa na Pep Gurdiola, tangu Pep apewe Barcelona kumechezwa jumla ya El Clasico 19, na hadi sasa Barcelona wameshinda 12, wamesuluhu 3 na kupoteza 4.
Lakini katika suala la makombe Barcelona nako wanaonekana kuburuzwa sana na Madrid, kwa ujumla Madrid ana jumla ya makombe 81(La Liga 33) huku Barcelona akiwa na jumla ya makombe 78 (La Liga 25).
Utawala wa Barcelona katika La Liga unaonekana kuanzia 1990/1991 ambapo kuanzia kipindi hicho hadi sasa Barca kabeba La Liga mara 15(Madrid mara 8), lakini Madrid Ulaya akiendelea kutamba mara 6 dhidi ya 5 za Barca katika kipindi hicho.
Tuje kwenye Ballon D’Or hapa sasa kila mmoja atawaza kuhusu Messi na Cr7 lakini kiujumla Barcelona wamewahi kutwaa tuzo hii mara 11 huku Madrid akibeba mara 10, lakini Messi na Cr7 wamebeba mara tano tano ni Johan Cruyff tu anayekaribia rekodi yao(3).
.
No comments